
MAREKANI: Rais wa zamani na Mgombea wa Urais kwa Chama cha Republican, Donald Trump alijeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi Julai 13 usiku, akiwa katika Mkutano wa Kampeni huko Butler, Pennsylvania, huku Msemaji wake akisema hali ya Trump inaendelea vizuri
Kupitia Mitandao ya Kijamii, Trump amesema alisikia risasi ikipita sehemu ya juu ya Sikio lake la Kulia huku shuhuda wa tukio akidai aliwataarifu Walinzi ‘Secret Service’ kuhusu mtu aliyekuwa juu ya Jengo na Bunduki lakini akapuuzwa
Katika taarifa ya awali, Rais Joe Biden amelaani tukio hilo na kushukuru kuwa Trump yuko salama


