
Klabu ya soka ya Simba imemtangaza Fadlu Davids kuwa kocha wao mkuu mpya akichukua mikoba ya Andelhak Benchikha aliyebwaga manyanga mwishoni mwa msimu uliopita.
Raia huyo wa Afrika Kusini mzaliwa wa Mei 21, 1983 alikuwa msaidizi wa Kocha Mkuu pale Raja Casablanca ya Morocco na anasifika kwa soka la pasi fupi fupi na uchezaji wa kujitoa.



