
“Miaka sita iliyopita nilikuja kwenu kama mgeni. Mlinipa kusudi na kunipa changamoto ya kuwa bora zaidi. Tuliteka ardhi hii pamoja, tukapanua eneo letu hadi sehemu zingine za Afrika na yaliyobaki ni historia. Baada ya miaka sita ya furaha kubwa, fahari, na malengo, hatima zetu zinachukua mwelekeo tofauti. Sina kitu kingine ila heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na msaada mliyonipa kwa miaka hii na hakuna mtu anayeweza kubadilisha historia tuliyoitengeneza pamoja.
Wanasema onyesho halijaisha mpaka mwanamke mnene aimbe na naamini wimbo huu unastahili muda wenu. Nawatakia kila la kheri na tutaendelea kuonana. Nguvu Moja.” – Ujumbe wa Clatous Chama kuiaga Simba SC



