
Simba SC imemshusha mshambuliaji raia wa Uganda, Steven Mukwala aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Simba ikijiandaa na michuano ya ndani na nje ya nchi Mukwala anatarajiwa kuwa suluhisho lao la kukosa mshambuliaji madhubuti kwa muda mrefu.



