Sativa Yuko Salama. Ataendelea na Matibabu Dar
Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa, kijana aliyetekwa na kupatikana Katavi huku akiwa na majeraha makali, ikiwemo jeraha la risasi ataendelea kupatiwa matibabu Dar es Salaam ambapo ataingia leo Juni 29,2023.
Ilitegemewa ataingia mchana wa leo kwa ndege ya ambulance, hata hivyo ratiba za usafiri zilibadilika na kwa sasa anategemewa kuingia usiku wa leo, ambapo ataelekea moja kwa moja hospitali.
Wadau mbalimbali walijitokeza leo mchana kwa ajili ya kumpokea katika viwanja vya ndege vya Dar, hata hivyo walijulishwa juu ya mabadiliko ya ratiba.



