

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Iringa wamegoma kufungua maduka huku sababu za mgomo huo zikiwa hazijawekwa wazi.
Mgomo kwa wafanyabiashara umeanzia katika Soko la Kariakoo, Dar es Salaam Juni 24, 2024 na kufuatiwa na Mwanza na Mbeya wakishinikiza Serikali kuwawekea mazingira rafiki ya kufanya biashara.



