
Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ali Kamwe amethibitisha kuwa klabu ya Yanga itakabidhiwa kombe la Ubingwa wa ligi Kuu ya NBC 2023/2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya 25/05/2024 ambapo pia siku hiyo watakuwa wakicheza mchezo wa NBCPL dhidi ya Tabora United.
Ally Kamwe amethibitisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Yanga SC Jangwani.



