
Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema haya
“Nimeshiriki mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia jijini Paris ulioandaliwa na Shirika la Nishati Duniani (IEA). Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu kutambulika kwa juhudi zetu katika eneo hili, na kupata nafasi ya kushiriki mjadala wa kimataifa kuhusu nishati safi ya kupikia ambapo majawabu yake yatawafaa watu bilioni 2.3 duniani wanaoishi na changamoto hii ya nishati, milioni 900 kati yao wakiwa katika Bara la Afrika. “
“Katika hotuba yangu nimeeleza dhamira ya nchi yetu kutekeleza mkakati wa kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa Miaka 10 tuliouzindua hivi karibuni wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030. Pia, nimeongeza sauti yangu kwa jamii ya kimataifa na wadau wa sekta hii kuongeza nguvu kisera na kifedha na kuufanya mwaka 2024 kuwa Mwaka wa Nishati Safi.”
Mabadiliko kuleta matumizi ya nishati safi ya kupikia ni hatua kubwa katika maendeleo ya watu wetu na yataakisi hatua tunazopiga kiuchumi na kwenye ukombozi wa mwanamke kwani hii ni moja ya changamoto kubwa kwao.
Tutafanikiwa.


