
Wakati msimu wa 2023/24 ukielekea ukingoni inadaiwa FC Barcelona ina mpango wa kumuuza Mshambuliaji wake, Robert Lewandowski mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake kuchukuliwa na Straika wa Liverpool, Darwin Nunez
Uamuzi huo umekuja baada ya Barcelona kushuhudia wapinzani wao wa jadi, Real Madrid wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga)
Lewandowski (35) amesaliwa na miaka miwili katika mkataba wake lakini Barcelona inataka kumuuza ili kupunguza gharama kubwa za mishahara ambazo klabu hiyo inapambana nazo



