
Baada ya Manchester City kuifunga Chelsea katika mechi 6 mfululizo zilizopita, hatimaye timu hizo zimetoka sare ya magoli 4-4 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge katika Premier League
Kutokana na matokeo hayo, Man. City imefikisha pointi 28 ikiendelea kubaki kileleni katika msimamo wakati Chelsea ipo nafasi ya 10 kwa kuwa na alama 16
Mara ya mwisho Chelsea kuifunga Man. City ilikuwa Mei 29, 2021 katika Fainali ya Champions League (1-0) baada ya hapo Chelsea ikapoteza mechi 6 zilizofuata pasipo kufunga goli hata moja


