
Timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imebeba ubingwa wa The African Football League 2023 kwa kuitandika Wydad Casablanca ya Morroco magoli 2-0 katika Fainali ya Pili.
Kutokana na matokeo hayo, Mamelodi imeshinda kwa jumla ya magoli 3-2 kwa kuwa katika Fainali ya Kwanza Wydad AC ilishinda magoli 2-1.
Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria umekamilisha safari ya Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza ilishirikisha timu nane ikiwemo Simba ya Tanzania


