
Hilo jengo linajulikana kama ‘Vauxhall Cross’ lipo mjini London kandokando ya mto Thames. Hapo ndipo yalipo makao makuu ya Shirika la ujasusi la Uingereza ‘MI6’. Ni shirika lililoasisiwa mnamo mwaka 1909 baada ya kutenganisha idara mbili za shirika la ‘Secret Intelligence Service Bureau’.
Idara moja iliundwa mahsusi kushughulika na ujasusi wa ndani ya uingereza ikifahamika kama MI5, huku idara nyingine ikihusika na ujasusi nje ya uingereza ikifahamika kama MI6 yaani ‘Military Intelligence section 6’ japokuwa watu hufanya makosa kwa kutamka ‘M sixteen’ badala ya ‘MI six’ wakidhani I ni 1.
Ifahamike kuwa ziliwahi kuwepo idara tofauti-tofauti ikianza na Military Intelligence section one ‘MI1, MI2, MI3, MI4, MI5,MI6, MI7, MI8, na MI9 hadi Military Intelligence section 19 MI19. Hizi zote zilifanya kazi katika vita ya kwanza ya Dunia hadi vita ya pili ya dunia mwaka 1919, ambapo baadae zilikuja kufutwa ama kujumuishwa katika idara zingine na kuacha MI5 na MI6 zikipiga kazi hadi leo hii.



