‐Ni rahisi zaidi kuzielezea hisia zako kwa mtu kwa vitendo kuliko kuzielezea kwa maneno hadi akuelewe.
-Uvivu unaambukiza, Ukiwa na ukaribu na mtu mvivu kuna uwezekano mkubwa na wewe ukawa mvivu kama yeye.
-“Furaha” huwa ni kazi kuifikia kisawa sawa sababu mara nyingi tatizo linapokuwa dogo ndivyo linakufanya ulifikirie zaidi’ kwa kuogopa baadae linaweza kuwa kubwa au litakuja kuleta madhara makubwa baadae.
-Wanaume huwa na kawaida ya kufanya maamuzi magumu na hatari zaidi kama kutakuwa na wanawake warembo karibu.
-Kulala mtupu (Uchi) husaidia kuongeza uwezo binafsi wa kujiamini.
-Kimo chako kina mchango mkubwa zaidi kwenye kujiamini, Watu warefu hujiamini zaidi tofauti na watu wafupi.
-Rafiki yako bora sio yule ambae mnatumia muda mwingi kuwa pamoja bali yule ambae mmetengeneza matukio mazuri pamoja.
-Haijalishi kwa hasira gani uliyonayo lazima utamsamehe tu mtu unaempenda.
-Kama unapenda kumkataza mtu kufanya jambo fulani ambalo wewe hupendi, Huwezi kumfanya kuacha Kupenda jambo hilo bali ataanza kukuchukia wewe



