Victor Osimhen: “Nimekuwa inspired na Sadio Mané. Lakini nina lengo tofauti ikilinganishwa na lake. Anajenga miundombinu kwa ajili ya watu wa kwao Senegal. Hilo ni jambo zuri.
Lakini kwangu mimi, nataka kuwasaidia watu wenye changamoto za ulemavu kote barani Afrika. Nitafanya kila niwezalo kusaidia pale ninapoweza kusaidia. Niko katika harakati za kufungua makao makuu barani Afrika ambayo yatanisaidia kufikia lengo hili.
Ikiwa mtu hana mguu, tutamuundia mpya. Ikiwa ni mkono, tutakuundia mpya. Tunataka wajisikie sawa na kila mtu. Tunafanya kazi kwa ajili ya Africa.”
Inapendeza, Victor! ✨



