
Victor Osimhen
Manchester United na Paris St-Germain zinapaswa kulipa ada ya uhamisho ya angalau £90m ikiwa zinataka kumsajili mshambuliaji mahiri wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, katika dirisha la msimu wa joto. (ESPN)
Arsenal wameweka kipaumbele cha kukubaliana kandarasi mpya na nyota wake Bukayo Saka, 21, na beki wa Ufaransa William Saliba, 21, huku Manchester City ikimtaka winga huyo wa Uingereza. (Sports)
Baada ya dirisha dogo la usajili Chelsea wameelekeza nguvu zao katika kuongeza mkataba wa Mason Mount, 24. Mkataba wa sasa kiungo huyo wa kati wa England unamalizika msimu wa joto wa 2024. (90min).

Mason Mount
Vyanzo vya karibu na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang vinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ameshtushwa na amesikitishwa kuachwa nje ya kikosi cha Chelsea cha Ligi ya Mabingwa Ulaya na anaamini klabu hiyo inataka kumuondoa. (Telegraph)
Manchester United wamekubali kuongeza mkataba wa miaka minne wa winga mwenye umri wa miaka 18 Alejandro Garnacho, ambaye amekuwa akifanya vizuri na kucheza timu za taifa za vijana za Argentina. (AS kwa Kihispania)
Wafanyikazi wa Old Trafford wamegawanyika kuhusu iwapo mshambuliaji wa England Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 21 aruhusiwe kuendelea na soka lake katika klabu hiyo ama la. (Guardian)
Greenwood anatazamia kuhamia China ili kuanza tena soka yake ikiwa United itaamua kumfuta kazi mara tu watakapokamilisha mchakato wao wa ndani.

Mason Greenwood
West Ham United na Everton watalazimika kusubiri hadi msimu wa joto kumsajili winga wa Suriname Sheraldo Becker baada ya Union Berlin kusita kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka mwezi Januari kwa sababu ya malengo yao ya Ligi ya Mabingwa. (Caught Offside)
Uhamisho wa beki wa kulia wa LA Galaxy Julian Araujo kwenda Barcelona umeshindikana baada ya Fifa kuamua kwamba nyaraka za kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ziliwasilishwa kwa kuchelewa mno. (ESPN)
Kiungo wa kati wa zamani wa Utrecht wa Marekani chini ya umri wa miaka 19 Taylor Booth, 21, anafuatiliwa na meneja wa Manchester United Erik ten Hag. (Mail)
Chanzo na BBC



