
Dirisha la uhamisho wa Ligi Kuu ya Uingereza litafungwa Jumanne saa 23:00 GMT – na kuna uwezekano wa mikataba ambayo inaweza kuongeza zaidi rekodi ya kiasi ambacho tayari kimelipwa.
Takriban £550m zimetumika mwezi huu, na kuvunja rekodi ya 2018 ya £430m.
Tarehe ya mwisho wa Ligi ya Soka ya Uingereza pia ni 23:00, wakati Scotland ni 23:59.
Bundesliga ya Ujerumani itafungwa saa 17:00, Serie A ya Italia saa 19:00, La Liga ya Uhispania saa 23:00 na Ligue 1 ya Ufaransa saa 11:59 – pia Januari 31.
Ligi Kuu ya Wanawake inafungwa saa sita usiku kwa uhamisho wa kimataifa na 17:00 kwa mikataba ya ndani.
Rekodi ya uhamisho ya Waingereza inaweza kuvunjwa katika siku ya mwisho ya uhamisho wa Januari kwa mara ya kwanza tangu 2011 wakati Chelsea ilipomsajili Fernando Torres wa Liverpool kwa £50m.
Chelsea wametoa ofa ya euro 120m (£105.6m) kumnunua kiungo wa Benfica kutoka Argentina Enzo Fernandez.
Muda wa Arsenal na wakati wa kumnunua kiungo wa kati wa Brighton Moises Caicedo unayoyoma huku dau la £70m likikataliwa.
Sean Dyche aliteuliwa kuwa meneja wa Everton siku ya Jumatatu atakabiliwa mikimbio ya dakika za mwisho ikiwa anataka sura mpya katika kikosi chake.
Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimetumia takriban pauni bilioni 2.5b msimu huu, ikijumuisha matumizi ya rekodi ya msimu wa joto ya pauni bilioni 1.9, mbali na rekodi ya awali ya pauni bilioni 1.86b mwaka 2017-18.
Kilichofanyika kufikia sasa
Mmiliki Todd Boehly’s Blues wametumia zaidi ya pauni milioni 200 kununua wachezaji saba wapya, akiwemo Benoit Badiashile (£35m), Andrey Santos (£18m), Joao Felix (kwa mkopo na ada ya £9.7m), Noni Madueke (£30.7m) na Mykhailo Mudryk (£62m ikipanda hadi £89m), wengi wao wakiwa na mikataba mirefu.
Kumekuwa na mabadiliko kidogo kutoka kwa vilabu vilivyo juu yao kwenye jedwali, lakini sio sana, huku Liverpool ikimchukua mshambuliaji wa Uholanzi Cody Gakpo kutoka PSV, Arsenal ikimsajili Leandro Trossard kutoka Brighton na Newcastle ikitumia pauni milioni 45 kumpata Anthony Gordon kutoka Everton.
Kumekuwa na ujio wa kuvutia Manchester United, huku mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst akijiunga kwa mkopo kutoka Burnley.
Inasemekana, kumekuwa shughuli nyingi miongoni mwa vilabu ambavyo changamoto kuu msimu huu ni kusalia kwenye ligi.
Wolves imekuwa na shughuli nyingi, ikiwasajili washambuliaji Matheus Cunha na Pablo Sarabia, kiungo Mario Lemina na beki Craig Dawson ili kuongeza kikosi cha Julen Lopetegui.
Nottingham Forest haijapunguza kasi yake baada ya majira ya kiangazi ambapo walisajili wachezaji 23, huku viungo wa kati wa Brazil Danilo na Gustavo Scarpa, na mshambuliaji Chris Wood, wakihamia City Ground mwezi huu.
Leeds walivunja rekodi yao ya usajili kwa kumsajili mshambuliaji Georginio Rutter na pia wamekubali dili la kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie kutoka Juventus kwa mkopo wa awali, wakati Bournemouth (Dango Ouattara kwa £20m), West Ham (Danny Ings kwa £12m) na Southampton (Mislav Orsic na Carlos Alcaraz kwa jumla ya £20m) wamehama.
Limekuwa dirisha gumu lauhamisho kwa Everton, ambao walimpoteza Gordon aliyetajwa hapo awali na kumuona Arnaut Danjuma akiwapa kisogo kabla ya kusajiliwa na Spurs muda mfupi baada ya kumfukuza meneja Frank Lampard.
Je, ni mikataba gani ipo mbioni?
Kama ilivyojadiliwa tayari, Fernandez na Caicedo ni walengwa wa uhamisho wa pesa nyingi hadi siku ya mwisho ya dirisha.
Taarifa za kushangaza ziliibuka Jumatatu kwamba beki wa pembeni wa Manchester City Joao Cancelo alikuwa kwenye majadiliano kuhusu uhamisho wa mkopo kwenda Bayern Munich ambao unaweza kusababisha uhamisho wa euro 70m (£61.5m) msimu wa joto.
Kiungo wa kati wa Stuttgart Naouirou Ahamada anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya uhamisho wa euro 11m (£9.7m) kwenda Crystal Palace, wakati kiungo wa Newcastle Jonjo Shelvey anazungumza na Nottingham Forest kuhusu uhamisho ambao utamfanya kuwa mchezaji wa 26 kusajiliwa msimu huu.
Wachezaji kadhaa wa michuano hiyo pia wamehusishwa na uhamisho wa Ligi Kuu, kama vile mshambuliaji wa Coventry Viktor Gyokeres, beki wa Stoke Harry Souttar na kiungo wa Sheffield United Sander Berge



