Tafakari yafuatayo

••Ni maisha yako,si yao. Wewe ndiye unayepaswa kuyaendesha.
••Ni vizuri kuwa na marafiki, lakini marafiki ambao wanataka kuyatawala maisha yako si marafiki wazuri.
••Maamuzi unayoyafanya leo yanaathiri maisha yako ya kesho,fikiri Kwa Makini kabla ya kufanya jambo.
••Kabla ya kutekeleza maamuzi yako,je,umetafakari athari zinazoweza kutokana na maamuzi hayo? Je, athari hizo zinaweza kukuinua au kukuzamisha?
••Fanya maamuzi ambayo yatakusaidia kutimiza ndoto zako.
••Ujinga ni umaskini– jitaftie maarifa ambayo yatakuza uwezo wako wa kufikiri na kutoa hoja.
••Uwe kiini cha mabadiliko wasaidie rafiki zako na wanarika wenzako wafahamu kwamba inawezekana na ni muhimu kwa mtu kufanya maamuzi yake mwenyewe.
••Kuna namna mbalimbali za kufanya mambo. Usijiskie kushindwa ikiwa njia moja ya kutatua imeshindwa kufanya kazi. Tafuta ufumbuzi mwingine
••Usiogope kueleza wazi msimamo wako juu ya jambo,inaweza kukusaidia wewe na wengine.••••



