Mwaka 2004 wakati 50 Cent akiwa kwenye ubora wake, kampuni ya kutengeneza kinywaji cha Vitaminwater kilitaka afanye tangazo na kukitangaza kinywaji hicho.
50 hakutaka kulipwa pesa yoyote ile bali aliwaambia alikuwa anahitaji share kwenye kinywaji hicho, wakakubaliana naye na kumpa kwani ndiyo kwanza ilikuwa kampuni changa.
50 akaanza kukitangaza mara kwa mara kiasi cha kupata wateja wengi. Mwaka 2007 kampuni ya Coca Cola ikanunua kinywaji hicho kwa kiasi cha dola bilioni 4.1, kwa kuwa 50 alikuwa na share yake, akalipwa kiasi cha dola milioni 100.
Ndiyo maana huwa nawaambia huyu ni muhuni mwenye akili sana



