
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kutokana na ukame unaoikumba Nchi ya Zambia, Serikali ya Nchi hiyo imeingia makubaliano na Tanzania kununua Tani 650,000 za Mahindi kwaajili ya kusaidia takriban Watu 7,000,000 nchini humo
Amesema Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha Miezi 8 na utaiingizia Tanzania Dola Milioni 250 (zaidi ya Tsh. Bilioni 650) na kuwa Mahindi hayo yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo kituo cha Songwe kitauza Tani 55,000, Makambako Tani 75,000, Sumbawanga Tani 250,000 na Songea Tani 270,000



