
➡️ Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matanshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) mbali na hili wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10
★ Kauli ya Ahmed iliyosababisha haya
➡️ “Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae , Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza ..mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”
➡️ “Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”
➡️ Demand letter ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao , hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini
➡️ Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)
1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake
2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 ( 10,000,000,000)
– Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi


