
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 07, 2024 ameendelea na ziara mkoani Iringa ambapo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iramba iliyopo katika kijiji cha Iramba, kata ya Itandula kwenye Halmashauri ya Wilaya Mufindi.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa shule hiyo Mheshiwa Majaliwa ameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kubaini vyanzo vitakavyoongeza fedha ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. “Ninawapongeza madiwani kwa wazo la kutenga fedha na kujenga mradi huu wa shule”
“Moja kati ya mapungufu ya baadhi ya halmshauri ni kutotumia fedha za ndani kujenga miradi inayoonekana, ujenzi wa shule hii ni mfano wa kuigwa na halmashauri zote, ongezeni kasi ya mkamilishe mradi huu kwa wakati”
Pia Mheshimiwa Majaliwa amewataka kutumia fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili miundombinu yote itakayojengwa iendane na fedha iliyotolewa.


