
Wafanyabishara wa soko kuu hapa Manispaa ya Mikindani wamegoma kufungua biashara zao kwa kile wanachoeleza kuwa ni kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara wengine unaoendelea katika maeneo ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam, Mbeya, Dodoma na Mwanza ambao unalenga kuishikikiza Serikali iyafanyie kazi madai yao 14 likiwemo suala la kamata kamata zoezi ambalo limekuwa likiendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kukithiri kwa utozwaji wa kodi.
Hii inakuja ukiwa ni siku mbili toka wafanyabiashara Kariakoo kuanza mgomo wao, jambo lililopelekea serikali kuja na masuala sita ikiwemo kusitishwa kwa operesheni kamata kamata.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekuta na uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara leo Juni 26,2024 ikitegemewa kwamba masuala mbalimbali yanayoibuliwa na wafanyabiashara yataenda kupata utatuzi.
Hadi sasa hakuna tamko lolote ambalo limetolewa na mamlaka husika



