IDDI Amin Dada Oumee, alikua raisi wa tatu wa Uganda, alitawala 1971 mpaka 1979, hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake wala hakuwahi kumruhusu mwandishi yeyote kuandika habari ya maisha yake. Hii inamaanisha hakuna uhakika ni lini na ni wapi alizaliwa.
Hakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1923 Koboko au Kampala. Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928, lakini hii imepingwa. Mwanawe Amin Hussein alisema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928. Mtoto wa Amin aitwae Hussein anasema baba yake alizaliwa Kampala mnamo mwaka 1928.
Fred Guweddeko wa Makerere University, anasema Idi Amin ni mtoto wa Andreas Nyabire alieishi kati ya 1889 na 1976. Nybire ni mmoja wa kabila la Kakwa ambalo lilibadili dini kutoka Ukatoliki kwenda Uisilamu mwaka 1910 na kubadili jina kuwa Amin Dada. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa



