1. Ukutane na watu wenye pesa na uwaombe pesa
2. Ukutane na watu wenye pesa uwaombe njia ya kutengeneza pesa
Ukutane na watu wenye pesa na uwaombe pesa
Mwalimu wangu wa marketing (masoko) aliwahi kusema kauli moja, kwenye maisha ukitaka kumuua mtu kiuchumi, mnyime njia ya kupata pesa alafu mpe pesa
Asilimia kubwa ya watu ambao wanaitaji pesa ni kubwa kuliko ambao wanaitaji njia ya kuweza kutengeneza pesa, ukimpa njia ya kutengeneza pesa hato tengeneza pesa
Bali wajibika katika kumpa pesa alafu mtumie yeye kujitengenezea pesa zako ndio kanuni kubwa ya matajiri dunia, Wana kunyima njia ya kutengeneza pesa na wanakupa pesa ili waendelee kukutumia kila kukicha.
Ukutane na watu wenye pesa uwaombe njia ya kutengeneza pesa
Uhitaji wa wengi ni kuitaji pesa lakini Sio namna ya kupata pesa (njia ya kupata pesa), maana Ake una wajibu wa kuwajibika kujua kwamba unaitaji nini unapo kutana na mtu mwenye fedha
Akupe njia ya kutengeneza pesa ama uwe kimya kwake ili uendele kuwa mwombaji wa pesa muda wote na kulalamika maisha magumu, asilimia kubwa ya watu wengi duniani, wanaikimbia njia ya kupata pesa Ila wako radhi waombe pesa, sababu ni uvivu wa kuitafuta pesa.



