Simba bado hawana kikosi bora cha kusema kikugarentii matokeo bora na Mpira kila mchezo kama walivyokuwa watani zao Young Africans kwa misimu iliyopita,
Ila kwasasa Simba ndio kinara wa ligi kuu ya NBC Huku watani zao Goung Africans wakijitafuta
SIMBA WAKISHINDA HATA GOLI 1 NCHI HUWA SHWARI.
Kipindi kama hiki Huwezi Kumsikia mashabiki wa Simba wakilalamika GSM kudhamini timu nane za ligi kuu,
Kipindi kama hiki Simba huwezi kuwasikia wakisema GSM ananunua marefa na anatuharibia ligi yetu,
Kipindi kama hiki Simba huwezi kuwasikia wakisema watahama ligi waende kucheza burundi,
Sasa hivi huwezi kuwasikia Simba wakiilaumu Tff kusema inaipendelea Yanga,
Wakati kama huu huwezi kuwasikia Simba wanamkataa Matola na kumtuhumu anawaharibia timu yao,
Kipindi hiki huwezi kusikia mwana simba akimtakaa Mwamuzi,
Kipindi kama hiki Simba huwezi kuwasikia wanamkataa Mzee Murtaza Mangungu na huwezi kuwaona wanaandamana barabarani wakimtuhumu Mangungu kuwa anawaharibia timu,
Kwasasa Wana Simba sasahivi wametiwa upofu kutokana na Yanga kufanya vibaya na wao kuendelea kupata ushindi wa papatupapatu,
Mashabiki wa Simba sasahivi hata ukiwaambia ukweli wanakuona huna akili wanaona unawawekea mchanga kwenye pilau
Furaha ya Simba inatokana na fomu mbovu ya yanga katika Michezo 2 ya ligi kuu iliyopita ila kuna muda utafika maji na mafuta Vitajitenga wenye timu bora watafurahia maisha na wenye timu mbovu ambao ni wataenda kulia na kunyoosheana vidole kukicha.


