Fahamu vyanzo vya tatizo,madhara yake na ufumbuzi wake.
Kwa wanaume tatizo la kuahirisha sana kazi za msingi huwa lina uhusiano mkubwa sana na homoni za testosterone ambazo humfanya mwanaume kuwa na nguvu za kiume, kujiamini,kujiona mwanaume Rijali,kujiona kiongozi,kuwa na nguvu na hamasa.
Upungufu wa homoni za testosterone husababisha upungufu wa nguvu za kiume ambapo husababisha uvivu, uzembe, kutegea,kulala sana, kutazama Tv muda wote,kupenda starehe sana kuliko kazi,kucheza video games muda wote,kukwepa majukumu,kukwepa ugomvi na migogoro,kuwa mpole sana,kuishi bila Mwenza kwa muda mrefu sana,kuridhika na hali ya maisha hata kama ni ngumu sana,mtu kujiona mdogo sana hata akiwa na miaka 45 anajiona mvulana wa miaka 18
Mwanaume ambaye anasumbuliwa na tatizo la uvivu, uzembe, kuahirisha sana kazi,kulala sana,kufanya kazi kwa kujisikia, matumizi mabovu sana ya fedha hujikuta akiwa kwenye migogoro ya kimapenzi ndani ya familia kwa sababu mwanaume ni kichwa cha familia na endapo kichwa cha familia hakiwezi kuwajibika ipasavyo husababisha Mwanamke kushika usukani na kuanza kumgombeza, kumfokea, kumdhalilisha, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia,kumtishia kumuacha mwanaume mara kwa mara.
Japokuwa wapo wanawake huamua kumkimbia mwanaume.
Mwanamke akiwa na tatizo la uvivu, uzembe, matumizi mabovu ya fedha, kuahirisha sana kazi, kulala sana, kufanya kazi kwa kujisikia anaweza kupewa msaidizi yaani house girl lakini kwa mwanaume haiwezekani.Kichwa cha familia hufanya maamuzi ya mwisho,hivyo mwanaume akiwa mvivu husababisha ugomvi na migogoro kila siku.
Ifahamike kuwa mwanaume ni kazi ngumu sana kwa sababu mwanaume hawezi kukwepa majukumu yake hata iweje lakini Mwanamke anaweza kupata usaidizi kama atakuwa na mwanaume imara ndani ya familia.
Soma ujumbe mpaka mwisho.
Tatizo la kuahirisha sana kazi (procrastination)ni tabia ya kusogeza mbele ratiba ya kazi,malengo, mipango mara kwa mara bila sababu zozote za msingi
.Kila mmoja huwa anasogeza mbele ratiba ya baadhi ya shughuli katika maisha ya kila siku lakini ikiwa imekuwa kawaida kwako kuahirisha sana kazi zako za msingi mara kwa mara bila sababu zozote za msingi huu ni ujumbe wako.
Unaweza kuahirisha ndoa, kurudi masomoni, kusafiri,kuzaa, kujenga,kununua bidhaa,kufungua biashara,kufanya mawasiliano na wazazi n.k lakini ile hali ya kuahirisha sana inakuja automatically bila kujizuia kwa mfano unaweza kujiona mpweke sana kwa sababu hauna mwenza kisha siku umempata mwenza mzuri sana mwenye kukupenda,kujali, kukuheshimu sana ghafla unaanza kumuona ni mbaya sana,unamuona amekosea mtu sahihi wa kujenga nae mahusiano, unaanza kumtafutia sababu za hapa na pale,unaanza kupuuza simu zake kisha akivunja mahusiano unaanza kumsumbua na kumuomba msamaha na endapo akirejea kwako unarudia vituko vilevile kila siku.
Kuishi na mwanaume au mwanamke mwenye kusumbuliwa na tatizo la kuahirisha sana kazi ni mateso makubwa sana kwa sababu hakuna kitu chochote cha maana mnaweza kupanga kwa pamoja kisha kifanyiwe utekelezaji.
ZIFUATAZO NI SABABU 4 ZA TATIZO LA KUAHIRISHA SANA KAZI
Sababu za kujitokeza tatizo la kuahirisha sana kazi ni kama ifuatavyo
1.MALEZI YA UTOTONI
Msingi mkubwa wa tatizo la kuahirisha sana kazi huanzia tangu utotoni.
Mtoto huwa anapata upendo na huruma kutoka kwa mama na vilevile huwa anafundishwa nidhamu,kufanya kazi kwa bidii,kutunza muda, umakini katika kazi kutoka kwa baba.
Kwa ufafanuzi wa eneo hilo tuangalie aina za malezi zenye kusababisha tatizo la kuahirisha sana kazi nyakati za ukubwani.
A.KUMPA MTOTO UHURU KUPITA KIASI (Absent of strong male role model)
Hapa ni aina ya malezi ambayo mtoto huwa yupo huru sana kula chochote, kuvaa nguo yoyote,kujenga urafiki na mtu yeyote,akifanya makosa hakuna adhabu wala karipio au onyo,
Mtoto anaweza kutoka nyumbani muda wowote na kurudi nyumbani muda wowote bila kuhojiwa chochote.
sababu ya uhuru kupita kiasi ni kukosekana baba imara ndani ya familia.Chanzo cha kumkosa baba imara ndani ya familia ni kifo cha baba, talaka, kutengana kwa wazazi, baba kufungwa gerezani, baba kuishi mbali sana na familia,baba kuitelekeza familia, kukataa ujauzito, kuhama makazi, kuathirika na dawa za kulevya, ulemavu, ugonjwa sugu, kucheza kamari, uhalifu,umri mkubwa sana,kuugua ugonjwa wa akili (kurukwa akili mpaka anafungwa kamba) hapa mtoto anapata malezi ya mama pekeake changamoto zake ni kwamba mama huwa anachanganyikiwa na kushindwa kumjengea nidhamu mtoto tangu mdogo.
Hapa mtoto anakuwa huku hajui namna ya kujipa muongozo yeye mwenyewe kwa sababu anakuwa yupo huru sana muda wote.
Ule uhuru kupita kiasi humuathiri kisaikolojia kwa kumfanya apende zaidi kufanya vitu rahisi na kukwepa kufanya kazi ngumu,hivyo akiwa mkubwa anakuwa hawezi kufanya maamuzi magumu kwa ajili yake au watu wengine kwa sababu hana mazoea hayo kwa muda mrefu.
Pale ambapo mtoto anakuwa huku haoni madhara yoyote ya kuacha kutimiza wajibu wake akiwa mkubwa haoni sababu yoyote ya kujenga NIDHAMU BINAFSI kwa sababu anajua akifanya au asipofanya kazi hakuna kitu chochote kibaya kinaweza kumpata.
Uhuru kupita kiasi utotoni husababisha tabia ya uvivu, uzembe,utoro,kutegea kazi nyakati za ukubwani.
Kama nyumbani hakuna mtu yeyote mchapakazi ni rahisi sana kuona kufanya kazi kwa bidii ni kujitesa.
Ikiwa nyumba nzima hakuna mtu wa kumfanya mfano wa kuigwa ni vigumu sana ukubwani kujua umuhimu wa nidhamu binafsi.
B.KUMLINDA SANA MTOTO (OVERPROTECTIVE PARENTS)
Sababu ya pili ya tatizo la kuahirisha sana kazi ukubwani ni kulelewa na wazazi au walezi ambao huwa wanamlinda sana mtoto muda wote.
(OVERPROTECTIVE PARENTS) wazazi wa aina hii huwa wenye kumharibu mtoto kwa kufanya kazi sana na maamuzi ambayo alitakiwa kufanya mtoto husika.
Tatizo hujitokeza kwa mzazi au mlezi kufanya assignment za mtoto badala ya mtoto kufanya assignment hizo,kumchagulia marafiki badala ya kumfundisha sifa za marafiki wema ,kumzuia kujumuika na watoto wengine,kujenga ukaribu uliopitiliza na mtoto,
Kumtawala mtoto idara zote,kumpangia kila kitu cha kufanya,kumzuia kufanya kazi yoyote au kumlazimisha kufanya kazi ngumu sana muda wote bila kumfundisha umuhimu wowote wa kazi hizo.
Kuweka sheria ngumu sana juu ya mtoto bila maelezo yoyote ya msingi,kumzuia mtoto kupata matokeo ya maamuzi yake mwenyewe muda wote,kumuepusha mtoto kuona madhara /matokeo ya tabia zake mwenyewe kwa muda mrefu sana.
C.KUMDEKEZA SANA MTOTO
Sababu nyingine ya tatizo la kuahirisha sana kazi ukubwani huanza kwa kupata malezi ya kudekezwa sana kwa muda mrefu sana.
Mtoto ambaye huwa anadeka sana hujifunza tabia ya uvivu, uzembe, utoro, kutegea kazi, ubinafsi, uchoyo,wivu,kisirani,kubeba chuki dhidi ya watu wengine ambao anahisi wanapendwa zaidi yake.
Mtoto ambaye huwa anadeka sana huona onyo kama unyanyasaji, kukosolewa pale amefanya makosa anaona ni udhalilishaji,anajifunza kususa mara kwa mara, anajifunza kulaumu wengine mara kwa mara
Anajifunza kujichukulia kuwa yupo juu ya sheria za ulimwengu,
Mtoto ambaye anadeka sana anakuwa amezoea akifanya makosa lawama anabeba mtu mwengine,akikosea hakuna onyo,akifeli lawama zinaenda kwa wengine,
Anazoea kuona maamuzi yake yote anafanya mzazi,anazoea kuishi kwa kutegemea maamuzi ya watu wengine hivyo akiwa mkubwa bila kugombezwa au kushinikizwa na mtu mwengine hawezi kufanya maamuzi yoyote.
Mtoto ambaye anadeka sana anazoea kucheza video games, kulala sana, kutazama Tv muda wote, kucheza muda wote, kutumia fedha nyingi sana bila kuhojiwa chochote hivyo akiwa mkubwa haoni madhara yoyote juu ya tabia zake hata kama watu wengine wanalalamika juu yake.
2.MSONGO WA MAWAZO
Sababu ya pili ya tatizo la kuahirisha sana kazi ni msongo wa mawazo.Unaweza kuwa umepitia malezi mazuri tu utotoni lakini endapo utakuwa unasumbuliwa na msongo wa mawazo utashindwa kufanya kazi kwa ufasaha badala yake utakuwa unaahirisha mara kwa mara.
Viashiria vya msongo wa mawazo ni
-Hasira kupita kiasi,hofu , wasiwasi, woga, kutetemeka sana,moyo kuuma sana,moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, kuchanganyikiwa
-Kulala sana mpaka unachoka au kukaa kitandani bila usingizi muda wote,kula sana au kupoteza hamu ya kula
-kuumia kooni,kupaniki,kujiona upo hatarini,kuona aibu,macho kuona ukungu, kupumua haraka haraka sana,mwili kuishiwa nguvu
-Kuumwa kichwa na mgongo, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu, kujuta, kutamani kujiua,hisia za kisasi,wivu kupita kiasi
-Kukosa umakini,kukosa maamuzi,hofu ya kufa ghafla,kujiona mgonjwa muda wote,hofu ya kukosolewa, hofu ya kusemwa vibaya
-Vidole kufa ganzi,kuumia begani na shingoni,kukosa hamasa ya kufanya kazi,kujihisi uchovu,kutokwa jasho viganjani
Unapokuwa na msongo wa mawazo akili hushindwa kufanya kazi kwa ufasaha na mara kwa mara unaahirisha kazi zako za msingi.
3.KUSHINDWA KUJIAMINI
(Imposter syndrome)
Pale ambapo unakuwa HAUJIAMINI kwa uwezo wako mwenyewe ni rahisi sana kufikiria namna ya kuahirisha kazi zako hata kama unaweza kufanikiwa eneo hilo.
Imposter syndrome huwa na viashiria vifuatavyo
-Kujiona haustahili mafanikio yoyote,kujiona mwenye uwezo mdogo sana kuliko watu wengine,kujiona utafeli hata ufanye bidii kiasi gani bado.
-Kujiona umefanikiwa kwa bahati tu,kushindwa kukubali pongezi,kuhisi watu wengine watagundua mapungufu yako na kuacha kukuamini
-Kushusha thamani mafanikio yako mara kwa mara hata kama unapewa pongezi,kujiona mkosaji muda wote.
Ukiwa na Imposter syndrome husababisha kukataa fursa za mafanikio kwa kuhisi haustahili mafanikio hayo.
4.MITINDO YA MAISHA (LIFE STYLE)
Sababu ya mwisho ya tatizo la kuahirisha sana kazi ni mitindo ya maisha kama ifuatavyo
Pale mtu akiwa mvivu sana au haipendi kazi yake ghafla hujikuta anatafuta njia za mkato ili kukabiliana na hisia mbaya ambazo huwa zinakuja mara kwa mara.
Njia za mkato ni kama vile kutazama video za ngono (pornography), kucheza video games, kulala sana, kutazama Tv muda wote,kula sana vyakula vyenye mafuta na sukari kupita kiasi,kula sana vyakula na vinywaji vikali vyenye kemikali nyingi sana,ulevi kupindukia, kujichua (masterbation),kutumia dawa za kulevya,kuvuta bangi, kutumia fedha nyingi sana kufanya starehe,kutumia simu muda wote katika mitandao ya kijamii, kucheza kamari,
Madhara ya njia hizo za mitindo ya maisha ni kusababisha unene kupita kiasi,msongo wa mawazo,kuingia madeni makubwa, kupoteza hisia za mapenzi,kufanya kazi chini ya viwango,
Kiafya mitindo hiyo ya maisha husababisha uwekezano wa kupata changamoto za kiafya kama vile kisukari, uvimbe, saratani, ugonjwa wa moyo,kuumwa kichwa na mgongo, kupooza,na maumivu makali sana ya mifupa.
UFUMBUZI WAKE
1.CHUNGUZA CHANZO CHA TATIZO LAKO
angalia chanzo cha tatizo lako kwenye vyanzo vinne hapo juu kisha kila chanzo huwa na ufumbuzi wake .
Weka malengo halisi (set achievable goal) kujiwekea malengo mengi sana husababisha kukata tamaa mapema kwa kuona hakuna mafanikio yoyote eneo lolote .
Malengo mengi hufanya unakosa utulivu sehemu zote.
2.KAA MBALI NA VISHAWISHI
Epuka kutazama Tv muda wote, kucheza video games, kula sana vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi,epuka kufanya masterbation,epuka ulevi, punguza kutumia mitandao ya kijamii muda wote,
3.BEBA MAJUKUMU
Kama hauna majukumu ni rahisi kujiona bado mdogo kiumri hata ukiwa na miaka 45 kama hauna mke au mme,hauna mtoto,hauna kazi yoyote ni rahisi kujiona bado mdogo sana unaweza kujiona upo na miaka 18 wakati upo na miaka 45.
Majukumu kuongezeka husababisha shinikizo la kufanya kazi kwa bidii kuongezeka na kuondoa tabia ya uvivu, uzembe,kutegea
4.EPUKA WATU WENYE TABIA AMBAZO HAUZIPENDI
Kama haupendi uvivu epuka watu wavivu,jenga ukaribu na wachapakazi,hupendi ulevi epuka watu wenye kutumia ulevi,haupendi uzembe kaa mbali na watu wazembe n.k
Ukianza kujiona umekuwa mfano bora wa kuigwa (Role model) ghafla tabia zako hubadilika kuendana na jina lako, lakini ukiona tabaka la chini tabia zako zitaendana na hali hiyo ambayo unajitambuliisha nayo.
Kama tatizo lako ni kubwa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya Counselling session na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu na utaona mabadiliko na kujisikia nafuu ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzo.



