Nakumbuka Kipindi Niko Mdogo Nilikuwa Nasumbua Sana Kuoga.
Siku Moja Bibi Akanambia Hivi,
“Tonny, Kama Ukioga Mapema Utasikia Baridi, Na Ukichelewa Kuoga Utasikia Baridi Vilevile.
Lakini Baridi Utakalosikia Kama Ukioga Mapema, Ni Tofauti na Utakalosikia Kama Ukichelewa Kuoga, Baridi Utakalosikia Ukichelewa Kuoga Linaweza Kuwa Mara 2 Hadi 3 Ya Lile Ambalo ungesikia Kama Ungeoga Mapema”
Maneno Yake Yanaishi Ndani Yangu Hadi Leo.
Na Yamenisaidia Kuwa Mtu ambae NACHUKUA HATUA MAPEMA.
Kuna Wewe Upo Katika Mahusiano, Unaona Kabisa Unatakiwa Kutoka Lakini Hutoki.
Kwa Sababu UNAKWEPA MAUMIVU.
Ukweli Ni Kwamba, Huwezi Kukwepa Maumivu. Kama Ukitoka Leo Utasikia Maumivu na Hata Ukitoka Miaka Kadhaa Ijayo Utasikia Maumivu Pia.
Lakini;
Maumivu Utakayosikia Kama Ukitoka Kwa Kuwahi Ni Tofauti na yale Utakayosikia Kama Ukitoka Kwa Kuchelewa.
Kubali Kuumia Leo Ili Ufurahie Uhuru Wako Kesho.
Kuliko Kujifariji na Kujivutavuta Leo Kisha Uje KUUMIA ZAIDI KESHO.



