
Tetesi zinasema kuwa Arsenal inakaribia kumsajili kiungo Moises Caicedo wa Brighton kwa ada ya uhamisho inayofikia £85m, wakitanguliza £75mil, baada ya ile ya kwanza ya £60m kukataliwa.
Kocha wa Brighton Robert De Zerbi amesema jioni hii kabla ya kuanza kwa mchezo wa FA Cup dhidi ya Liverpool: “Moises ni mtu mzuri. Kwenye maisha kuna kukosea. Ziko njia nyingi za suluhisho kwa kila mtu, tutaona njia gani nzuri kwa klabu, kwakwe na sie.”
Weston McKennie anaelekea Uingereza sasa kukamilisha uhamisho wake kutua Leed United. Kesho atapimwa afya kabla ya kuweka saini mkataba wake wa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu akitokesa Juventus. (David Orstain)

Chelsea imemtangaza kumsajili beki wa kulia wa Lyon Nalo Gusto ambaye ataendelea kusalia Ufaransa kwa mwisho mwa msimu. Lakini haijamaliza usajili ikiwasaka viungo Moises Caicedo wa Brighton, Amadou Onana wa Everton na Enzo Fernandez wa Benfica na mshambuliaji Marcus Thuram wa Borussia Monchengladbach. (Chelsea)
Chelsea pia inataka kumpa mkataba mpya kiungo wake Mason Mount ambaye ataingia kwenye rada za Liverpool katika dirisha lijalo la usajili. Liverpool ‘wanamzimia muingereza huyo ambaye amesalia na miezi 18 katika mkataba wake wa sasa na Chelsea. (Skysport)
Mount

Leicester imekamilisha usajili wa winga wa Brazil Mateus Tete kwa mkataba mfupi mpaka mwishoni mwa msimu.
Mbrazil huyo alikuwa na Lyon, na anaruhusiwa kusaini mikataba mifupi mifupi kutokana na mzozo wa vita huko Ukraine ambapo klabu yake ya Shakhtar Donetsk inatokea. (Skysport)





