
Meneja wa Rasilimali za Mawasiliano na Usimamizi wa Teknolojia wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Robson Shaaban, akifungua warsha ya siku mbili (2) kwa Watoa Huduma za Mtandao wa Intaneti (ISPs), Watoa Huduma za Simu za Mkononi (MNOs) na Taasisi za Serikali iliyofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 June 2024 katika ofisi za TCRA, Dar es Salaam.
TCRA imeshirikiana na Chama cha Watoa huduma za Mtandao wa Intaneti (TISPA) kuendesha warsha hiyo yenye dhumuni la kubadilishana uzoefu wa kiufundi kuhusiana na masuala ya usimamizi na uendeshaji wa mifumo na mitambo pamoja na kuboresha ulinzi na mwingiliano katika upatikanaji wa huduma ya mtandao.
Hizi ni kati ya hatua zilizochukuliwa na TCRA katika kujenga ustahimilivu na upatikanaji wa huduma muhimu zinazopatikana na kuhifadhiwa nchini pindi panapotokea hitilafu au majanga kama kukatika kwa mkongo intaneti wa baharini.



