
Simba Yajipanga Kabla ya Dabi ya Kariakoo Yanga vs Simba Ligi Kuu NBC
Kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC, Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC, wachezaji na kocha wa Simba wameeleza malengo yao na maandalizi wanayofanya kuhakikisha wanapata matokeo chanya.
Shomari Kapombe, mchezaji wa Simba, alisema:
“Malengo yetu ni kuwa mabingwa wa Ligi, tunajua tupo nyuma kwa alama nyingi lakini tumejiandaa kupata alama tatu kesho ili kupunguza tofauti ya alama, kwa maandalizi tuliyofanya, wasimba watafurahia uwepo wetu hapa Zanzibar.”
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, pia aliweka wazi mkakati wa timu:
“Yaliyopita yamepita, kesho tutapambana kuhakikisha tunabadili hiyo rekodi ya kufungwa. Hii ni mechi kubwa yenye presha kubwa kwasababu tunaenda kucheza na timu kubwa, tutajiandaa ili kupunguza presha kwa wachezaji.”
Mechi ya Dabi ya Kariakoo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya timu zote mbili na shabiki wengi kutarajiwa kufuatilia pambano hili. Simba SC inatarajia kuendeleza maandalizi yaliyowekwa ili kuhakikisha wanapambana kwa ushindi na kuendelea kushika nafasi nzuri kwenye Ligi Kuu ya NBC.




