
️-Sikuwahi hata kuwaza kama kuna siku nitakuwa kiongozi wa klabu kubwa ni kitu ambacho kimetokea kutokana na mfululizo wa matukio ambayo yamefanya leo nimekuwa kiongozi wa Yanga.
Nilikuwa mwanachama, baada ya hapo GSM ilipoingia katika uwekezaji na Yanga ndipo nikapendekezwa kuwa Rais wa Yanga”
️-Yanga ni taasisi kubwa hapa nchini,na ina taratibu zake pia kuhusu mchezaji Feisal salumu sisi Kama Viongozi hatuwezi kumwonea huruma hata kidogo kwasababu tulishampa nafasi ya kuja klabuni kuendelea kutumikia mkataba wake hadi mwisho,,Tulimpa nafasi ya kuja kuendelea na mazungumzo kwa ajili ya kuboresha maslahi yake,,na mwisho Tulimpa nafasi aje klabuni tuzungumze kuhusu ada ya usajili kwa timu yoyote ambayo inamuhitaji Feisal.

Lakini hakuna ambacho amekitekeleza Feisal,Bado tunaendelea kumlipa mshahara wake Kama kawaida ila mwisho wa jambo hili sisi Viongozi hatutakuwa na huruma nae pale na sisi tutapopigania haki yetu Kama taasisi.
-Mimi ndio niliekwenda Accra Ghana kumtafuta Bernard Morrison baada ya kocha Luc Emery kunambia juu ya uwezo wake, Najivunia sana kumwona Bernard Morrison yupo nasi kwa sasa licha ya matatizo ambayo yalitokea baina yetu na yeye.

️-Kwa ukanda huu wa afrika mashariki na Kati hakuna klabu ambayo ina wanachama wengi na mashabiki kuizidi Yanga sc na hii sisemi kiushabiki,Ila sisi Kama Yanga tuna database ambayo tunaweza kukupa ukaona idadi ya wanachama hai ambao wamejisajili kwenye mfumo wetu mpya wa mabadiliko.
️Kuna kauli ambazo zipo mitaani kuna watu wanajiita watu wa mpira, hawako kama sisi ma-Engineer ambao tumeenda shule lakini wao sijui wanarasimishwa na nani! Nataka niwaambie hili, Football Club haiendeshwi na Watu wa Mpira, inaendeshwa na Taaluma na nadhani hilo ndio limefanya kwa kiasi kikubwa tuchelewe kufanikiwa katika vilabu vyetu”
“Unahitaji mtu sahihi kwenye kila idara ili kuiendesha idara husika kiusahihi lakini kwa sisi Yanga nje ya taaluma moja kati ya vigezo vyetu ili tukuajiri ni lazima uwe mwanachama wa Yanga”
️-Jumapili hii tunakwenda kuweka historia Yanga kuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania kucheza fainali ya CAF CONFEDERATION CUP ,,Kuna watu wanasema walicheza fainali Kama ambayo hii sisi Yanga tunakwenda kucheza Ila ukweli wanao ni kuwa wao walicheza fainali ya CAF CUP ambayo hayo mashindano hayapo yalikoma toka zamani


