
Ambapo amesema kuwa
Ikiwa ni miaka 25 tangu kuundwa tena kwa Jumuiya hii muhimu kwa maendeleo ya nchi zetu, nimeeleza moja ya kazi tunazofanya katika kuimarisha hali ya maisha ya wananchi wetu kupitia sekta ya nishati. Katika mjadala, nimeshirikisha jitihada zetu kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hapa nchini, ikiwemo hatua kubwa na ya kihistoria tuliyofikia kwa ukanda huu wa Afrika ya kufikisha nishati ya umeme kila kijiji.

Nimewasihi viongozi wenzangu kuunganisha sauti zetu pamoja, na kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha upatikanaji nafuu na wa uhakika wa nishati safi ya kupikia kwa wananchi wetu. Hatua hii ni sehemu ya kazi njema katika kuinua hali zao za maisha, na kujenga msingi katika utunzaji wa mazingira, jambo ambalo ni muhimu kwa ustawi wa Jumuiya yetu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.



