
Aliyekuwa kiungo kipenzi cha wananchi, Mukoko Tonombe, amepata bandari mpya! Baada ya misukosuko ya usajili nchini Algeria, kiungo huyo wa kimataifa wa DR Congo sasa amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Jableh SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Syria.

Mukoko ameamua kuelekea Syria baada ya dili lake la nchini Algeria kukwama kufuatia sheria za shirikisho la soka la nchini humo.
Tonombe anakumbukwa zaidi nchini Tanzania kwa uwezo wake mkubwa wa kumudu eneo la kiungo alipokuwa akiitumikia Young Africans SC (Yanga). πΉπΏ



