
Hatukucheza vizuri kama tulivyotaraji, tulifanya mazoezi vyema na kuiandaa mbinu tuliyoanza nayo leo lakini wachezaji walishindwa kufanya kama tulivyowafundisha na kuwaelekeza mazoezini,” alisema Nabi na kuongeza;
“Pamoja na yote tunashukuru kwa ushindi na sasa tunarudi kujipanga na mechi ya maruduano tunayoamini itakuwa ngumu ugenini ila tunahitaji matokeo yatakayotufanya kutinga fainali.”
Baada ya mechi ya leo, Yanga itarudiana na Marumo, Mei 17 mwaka huu mchezo utakaopigwa nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo huo, Yanga inahitaji ushindi au sare ili iweze kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.



