
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, umewasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la kuagwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na viongozi mbalimbali wa kitaifa, ndugu, jamaa, na wananchi katika kutoa heshima za mwisho kwa Dkt. Ndugulile, ambaye atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya na utumishi wa umma.
Ratiba hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, wawakilishi wa vyama vya siasa, pamoja na wananchi waliokusanyika kuonyesha heshima zao za mwisho.


