
Spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Namibia; ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM), Mhe. Dkt. Anne Semamba Makinda, ameelezea kuridhishwa na uchaguzi mkuu wa Namibia uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 na kukamilika mapema leo tarehe 28 Novemba 2024, ambapo ulikuwa wa amani na utulivu.
Mhe. Dkt Makinda ameyasema hayo katika ufunguzi wa vituo vya kupigia kura, ambapo alishuhudia zoezi la upigaji kura katika kituo cha A-Shipena Sekondari kilichopo katika jimbo la John A. Pandemi lililopo katika mkoa wa Khomas nchini Namibia.
Dkt Makinda amesema kwa vituo kadhaa alivyovitembelea mkoani Khomas hadi usiku wa kuamkia leo, vimeonesha mazingira ya utulivu, amani na usalama kwa wapigakura wote kwani walikuwa wamejipanga mistari pasipo na fujo, wakisubiri kuitwa kwa zamu, ili wakapige kura.
βNimefurahishwa kuona utulivu wa namna hii



