How do you express your gratitude?

Tanzania na Msumbiji ni ndugu na washirika tangu harakati za ukombozi wa nchi za Afrika toka kwa utawala wa kikoloni, nchi yetu ikitoa mchango mkubwa wa ukombozi wa Msumbiji. Kihistoria, chama cha FRELIMO kilichowaongoza wananchi kufikia uhuru wa Msumbiji kilianzishwa jijini Dar es Salaam tarehe 25 Juni mwaka 1962, na ndipo yalipokuwa makao yake makuu hadi mwaka 1975.
Ikiwa ni sehemu ya matunda ya uhuru, nchi zetu hizi sasa zinaendelea na kazi ya kukuza uhusiano wetu ili kuongeza tija katika maeneo yanayoboresha maisha ya wananchi wa pande zote mbili, hasa maendeleo ya kiuchumi.



