Kuna mtu anaitwa Mole, huyu ni afisa usaliti, yaani anaweza kuwa miongoni mwenu, anachukua taarifa zenu na kupeleka kwa maadui, ilitokea sana hii kwenye vita baridi baina ya Marekani na Urusi.
Sasa bwana siku moja CIA walihisi kulikuwa na siri zao nyingi zilikuwa zinavuja na kwenda kwa Warusi, wakahisi kabisa mulikuwa na mtu ndani ambaye alikuwa anachukua taarifa na kuzipeleka kwa maadui zao.
Walichokifanya ni kuanza uchunguzi, wakaamua kumchukua ajenti wao, Robert Hanssen kwa ajili ya kuchunguza ni nani alikuwa mole ndani ya CIA.
Baadaye wakagundua huyo Robert ndiye alikuwa mole mwenyewe na alianza kufanya kazi na Warusi tangu mwaka 1979. Aligundulika mwaka 2001.



