
Leo Februari 2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Simba watakuwa wageni wa Tabora United inayopasua vichwa vya timu kubwa msimu huu wa Ligi Kuu NBC.
Simba inasafiri kwenda Tabora ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wao wa raundi ya kwanza kwa goli 3-0, ila pia inashuka dimbani ikiwa na tahadhari kubwa ikitambua kwamba timu kubwa tatu kwenye ligi zimepoteza dhidi ya warina asali hao wa Tabora nazo ni Yanga, Azam na Singida Black Stars.
Simba inafahamu ushindi pekee ndio utaifanya kurudi na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kushushwa na Yanga hapo jana wakipata alama tatu dhidi ya Kagera Sugar, tangu Tabora ipande daraja haijawahi kuifunga Simba, msimu uliopita ilipasuka nje ndani kwa goli 4-0 kisha 2-0.



