
Baada ya Elie Mpanzu kusaini mkataba wa miaka miwili (2) na Klabu ya Simba, nyota huyo amesema hakuwa na mpango wa kuwasaliti Simba kutokana na upendo mkubwa ambao ameoneshwa na mashabiki wa klabu hiyo wakati akipitia kipindi kigumu katika majukumu yake Uwanjani.
Mpanzu ameeleza hayo kupitia mtandao wake wa Instagrama, ambapo ameandika kuwa;
”Ninyi ndio wafuasi bora zaidi ambao nimewahi kukutana nao. Nataka kuwashukuru kutoka moyoni mwangu kwa msaada wenu usioyumba, licha ya nyakati ngumu ambazo nimepitia. Mmekuwa mkiniamini kila wakati, Ndiyo maana nimeamua kutowasaliti na kuendelea na klabu.”
Nyota huyo raia wa DR Congo tayari msimu kwenye ligi kuu amefunga magoli mawili (2) na kutoa assist tano (5) huku akiisaidia Simba SC kupanda mpaka nafasi pili kwenye msimamo wakiwa na alama 31 katika michezo 14, ikiwa ni tofaut ya alama saba dhidi ya Vinara Yanga wenye alama 38.





