
MICHEZO: Timu ya Simba imeutafuna mfupa ambao ulimshinda mpinzani wake wa Jadi (Yanga), hiyo ni baada ya kuikandamiza Tabora United magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi katika Ligi Kuu Bara
Magoli mawili kutoka kwa Leonel Ateba na moja la Shomari Kapombe yameiwezesha Simba kufikisha pointi 43, hivyo kurejea katika usukani wa Ligi ikiishusha Yanga yenye alama 42, timu zote zikiwa zimecheza michezo 16
Tabora United ambayo iliifunga Yanga magoli 3-1 imebaki na alama 25 ikiwa nafasi ya Tano katika michezo 16 pia



