MANYARA: Timu ya Fountain Gate imeilazimisha Simba sare ya Goli 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Matokeo ambayo yanaifanya Simba ibaki nafasi ya pili katika Msimamo waLigi kwa kuwa na alama 44 nyuma ya Yanga yenye pointi 45
Timu ya Simba ilianza kufunga kupitia kwa Leonel Ateba dakika ya 57 lakini Fountain Gate ambayo imefikisha alama 21 ilipata goli kupitia kwa Ladack Chasambi aliyejifunga dakika ya 75



