
Mahakama yaamuru Asamoah Gyan(37) amlipe fidia aliyekuwa mke wake nyumba 2, moja ikiwa nchini Uingereza na nyingine ikiwa Accra, Ghana, pia ampe kituo kimoja cha biashara ya petrol na gari mbili. Ni baada ya vipimo vya DNA kubaini kweli yeye ndie baba halisi wa watoto 3 aliokuwa akiwatilia shaka kuwa sio wake kwa madai aliyekuwa mke wake alichepuka
Gyan ambaye kabla ya kustaafu soka mwaka huu aliwahi kuwa Captain wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya nchini Ghana kisha kuchezea klabu kadhaa ikiwemo Sunderland, yeye ndie alitaka ndoa yao waliofunga mwaka 2013 ivunjwe.
Nyumba ya Aacra, Ghana aliyopewa ex wake huyo imeelezwa ilinunuliwa kwa ajili yake kabla/walipokuwa wakielekea kufunga ndoa yao 2023
Pia mahakama imeamuru kila mwezi Asamoah atoe pesa za matumizi kwa ajili ya watoto wao watatu £1,729 ambazo sio chini ya shilingi milioni 5.2 za Kitanzania
Kwa mujibu wa taarifa, inadaiwa kwamba mahakama ilieleza kuwa mama watoto wake huyo kwa jina la Gifty hakuwa na mchango wa moja kwa moja wa kipesa katika mali za mume wake, isipokuwa ndie alikuwa muangalizi na mlezi wa watoto wao 3 na hivyo mwanasoka huyo kwa upande wake yeye kupata muda wa kutosha kuweza kujiimarisha na kutimiza ndoto zake katika ulimwengu wa soka na kuchanua kiuchumi wakati mkewe akiwa anakomaa kulea watoto wao


