
Rais Samia Suluhu Hassan Mapema leo amezindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni, Jijini Dar es Salaam.
Ambapo amesema
“Tunaendelea kupiga hatua kubwa katika kukuza sekta ya viwanda, na ninapata faraja kubwa kuona wananchi hasa vijana wakinufaika na fursa zitokanazo na mafanikio haya. Maendeleo haya hayakuzi uchumi wetu kwa ajira za viwandani pekee, bali pia ajira zitokanazo na sekta nyingine, kwani tumekusudia kuona viwanda hivi vinatumia malighafi nyingi kutoka ndani ya nchi yetu ikiwemo rasilimali watu. “
“Hatua hizi ni za kujivunia kwa nchi yetu na zinatusukuma mbele kuendelea na kazi ya kuboresha mazingira ya kukuza uwekezaji wenye tija kwa wananchi ikiwemo; kuendelea kuweka mazingira rafiki ya mahusiano kati yetu na jamii ya kimataifa pamoja na kuwa na mifumo ya kikodi yenye unafuu hasa pale uwekezaji unapokuwa katika hatua za awali.”



