Mahitaji:
1. Papai bichi
2. Samli safi (ghee) – inapendekezwa kutumia ile ya asili, kama Tanga Fresh
Namna ya Kuandaa:
1. Safisha papai bichi, menya vizuri na toa mbegu zote.
2. Chemsha papai hilo mpaka lilainike.
3. Saga (blend) papai kisha acha ipoe.
4. Changanya papai uliosaga na samli safi kwa uwiano sawa.
(Mfano, kikombe 1 cha papai kwa kikombe 1 cha samli safi)
5. Tumia vijiko viwili (2) vya mchanganyiko huu, mara tatu (3) kwa siku.
Muda wa Matumizi:
Endelea kutumia tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja.
Utaanza kuona mabadiliko baada ya wiki moja.
Uhifadhi:
Hifadhi mchanganyiko huu kwenye friji.
Tayarisha mchanganyiko mpya kila baada ya wiki moja.
Kumbuka:
Tiba hii ni ya asili na matokeo yanaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.
Kama hautaona nafuu baada ya muda uliopendekezwa, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa afya au daktari.



