Goal Setting : Jinsi ya kufikia malengo yako chuoni

Kitu kimojawapo ambacho natamani kuwa ningekifanya kabla sijaenda chuoni ni kuweka malengo. Malengo ambayo ningetaka niyatimize katika miaka yangu ya chuo, miaka minne ambayo nilikuwa chuo. Nadhani hatuweki malengo ili tubanwe Ila ili tuwe na nidhamu.
Malengo yanasaidia kukupa self control na kukupa kitu unacho aim, na hivyo badala ya kuishi tu bila direction na kupoteza muda unakuwa na kitu kinachokuongoza namna unavyoishi.
So kwavile Mimi sikuwa na wazo hili toka hapo, nataka kushare na wewe aina za goals ambazo naona kama mwanachuo unayeenda kwa Mara ya kwanza zitakusaidia sana. Panga goals zako kabla haujaenda, ili uende ukiwa tayari na mpango wa kuzitimiza.
Fahamu : Mambo 5 ya msingi ya kuyafanya pale boom linapoingia
Goals zenyewe ni;
– Financial goals
Hapa kwenye pesa utakazopata, boom lako unapanga kulitumiaje? Je, matumizi yako yakipesa yatakuwaje? Je, unatamani kuanzisha biashara? Unatamani hela uliyonayo ikuingizie zaidi? Nk
Jiweke malengo vile unataka financial situation yako iwe.
Fahamu : Jinsi ya kubajeti boom ili likae muda mrefu
– Academic goals
Hapa weka malengo kuhusu masomo yako, unatamani ufaulu wako uweje, utasomaje, matumizi ya resources za chuo and etc. Unapoenda chuo kwa miaka yako unayoenda, unatamani kufikia wapi academically? Na sio lazima liwe jambo la kutisha, weka realistic goals ambayo unaweza kuzifikia.
Hapa niongezee na professional goals…. Unataka kujifnza chochote kipya ukiwa chuo? Na je akati upo chuo utajiendelezaje professionally au kujiendeleza kwa kile unachokisoma nk.
Fahamu : Jinsi ya kuandaa ratiba binafsi ya kujisomea kwa ufanisi chuoni
– Personal goals
Binafsi unatamani uweje? Ukue katika eneo gani as a person? Ujifunze kitu gani kipya ukiwa chuo? Unataka ufanye sports, ufanye mazoezi, ule balanced diet or how will your personal life be like?
Hapa niongezee na relationship goals, unaweza kuongezea vile unatamani kurelate na watu au hata kuyaendesha maisha yako kwenye mambo ya kijamii(social life).


