
Siku kama ya leo,28.6.1914, Franz Ferdinand, Mrithi wa taji la kifalme katika dola la Austria-Hungary pamoja na mke wake Sophia waliuwawa kwa kupigwa risasi na kijana wa ki-serb,Gavrilo Princip.
Ferdinand alifika Sarajevo katika ziara ya kukagua usalama na maendeleo ya himaya.
Shambulio hili lilipangwa kwa ustadi mkubwa na Danilo Ilic aliyekuwa mwanaharakati katika kikundi cha “Black Hand” kilichoazimia kupata uhuru wa Wa-serb kutoka katika dola la Austria-Hungary.
Ilic aliitambua vyema βrouteβ atakayotumia Ferdinand na kisha akaandaa vijana sita aliowapanga katika maeneo tofauti kwa ajili ya kutekeleza shambulio.Nderemo za wananchi waliojipanga kando ya barabara kwa ajili ya kumpokea zilimfanya Archduke Ferdinand aamini yupo mahala salama.

Gari la Ferdinand likafika kwa mshambulizi wa kwanza,Mehmedbasic,akaingia hofu na akashindwa hakufanya shambulio.
Woga pia ukamvaa mshambulizi wa pili, Vasco Cubrilovic ,aliyekuwa amejihami kwa pistol na bomu la kurusha kwa mkono.
Msafara ukamsogelea mshambulizi wa tatu,Nadeljko Cabrinovic,hakufanya ajizi,akarusha bomu katika gari ya Ferdinand kwa bahati nzuri bomu likagonga gari kwa nyuma na kulipuka mbali na gari ya Ferdinand na kujeruhi watu zaidi ya 20.
SOMA PIA: JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI.
Cabrinovic akanywa sumu ya Cynide na kujitupa mtoni ili kupoteza maisha na kufuta ushahidi,kwa bahati nzuri au mbaya sumu haikufanya kazi kwa kuwa ilikwisha-expire,polisi wakamuopoa na kumkamata Cabrinovic kutoka majini.
#Sikio_la_kufa_halisikii_dawa!

Punde tu baada ya shambulio,msafara ukakimbizwa sehemu yenye usalama lakini muda mfupi baadaye Archduke Ferdinand akakataa ushauri wa kuahirisha ziara na akataka atembelee wahanga wa shambulio waliokuwa wakipatiwa matibabu hospitalini.
Kosa kubwa lililofanywa ni kupita katika njia ile ile ya mwanzo palipofanyika shambulio la awali.
Gravrilo Princip,mmoja ya vijana 6 walioandaliwa kwa ajili ya shambulizi hakuwa amekata tamaa na bado alikuwako eneo la tukio akiwa na silaha yake,ghafla akauona msafara umefika mahala alipokuwapo.

Wanausalama walipogundua wamefanya kosa,wakamwamuru dereva asimamishe gari ili kubadili njia ya msafara.Hiyo ndiyo fursa Princip alikua akiusubiri muda wote,akachomoa pistol yake na kumimina risasi kwa Archduke Ferdinand na mkewe Sophia,punde tu wakakata roho kutokana majeraha ya risasi zilizopigwa na Princip.
Kufuatia kifo cha Archduke Ferdinand,Austria ikatangaza vita dhidi ya Serbia,Urusi ikajitokeza kuisadia Serbia.Ujerumani ikaiunga mkono Austria na kutangaza vita dhidi ya Urusi na kisha kuvamia Ufaransa na Ubelgiji.Uingereza ikaingia vitani dhidi ya Ujerumani,Vita ikasambaa dunia nzima.

Katika ardhi ya Tanganyika vita hii ilipiganwa katika maeneo tofauti,mapigano makali yakitokea kwa mara ya kwanza mkoa wa Tanga,vita inayofahamika kama “Battle of Tanga” au “Vita vya nyuki” ambapo Ujerumani ilitoa kipigo cha mbwa-koko kwa Mwingereza.
Princip akiwa gerezani alijutia kitendo alichofanya kwa jinsi kilivyochochea vita iliyokuja kugharimu maisha ya watu zaidi ya milioni 15 kote duniani.
Please subscribe and share our website for more fun and knowledge



