
Inawezekana kabisa ukawa hufahamu hili,lakini ndiyo ilivyo.
Nchi ya Korea Kaskazini ambayo jina lake rasmi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) ina sheria maalumu iliyothibitishwa na serikali ambayo inayoelekeza aina ya mitindo ya nywele kwa wanawake na wanaume wa nchi hiyo ya Kijamaa.
Jarida la Time la Marekani liliwahi kunukuu gazeti la Telegraph mwaka 2013 kuwa katika nchi ya Korea Kaskazini wanawake wameruhusiwa kuchagua mitindo 14 iliyoidhinishwa na serikali ya nchi hiyo ambapo wanawake walioolewa wameelekezwa kuwa na nywele fupi huku wale wasioolewa wameelekezwa kuwa nywele ndefu, zilizomwagika na zilizojisokota.
Wanaume pia wana mitindo yao 14 iliyoidhinishwa na serikali ya nchi hiyo.
Wanaume wamekatazwa kufuga nywele zaidi ya sentimita 5 au nchi mbili wakati huo huo wazee/watu wazima wameruhusiwa kufuga nywele kwa urefu usiozidi sentimita 7 (nchi 3)
Inaelezwa kuwa sheria hii imeleta usawa katika mitindo ya nywele baina ya wanawake na wanaume nchini Korea.
Mwaka 2005 gazeti la Daily Mail liliwahi kuripoti kuwa televisheni ya Taifa ya Korea iliandaa vipindi maalumu vya muendelezo (series) vinavyoelekeza namna ya ukataji wa nywele na mitindo mbalimbali ya ukataji nywele kwa style ya kisasa ya kijamaa.
Lakini mwaka 2017 gazeti la Daily Mail liliripoti tena kuwa katika nchi ya Korea Kaskazini wanawake wana style 15 za mitindo ya nywele na wanaume pia wana style 15 za mitindo ya nywele.
Katika aina hizo za mitindo ya nyweke kuna aina mbili za unyoaji ambazo zimewekwa kwa kundi maalumu.
Katika mitindo hiyo kuna mtindo maalumu wa nywele ambao unanyolewa na kingozi wao nchi hiyo tu Mwenyekiti Kim Jong Un na kuna mitindo kwa ajili wanajeshi, walimu, wanafunzi na kundi maalumu la viongozi n.k.
Iliwahi kuripotiwa kuwa mwaka 2015 Kim Jong Un aliwaagiza wanaume kuiga mtindo wake wa lakini akiweka angalizo kuwa nywele hizo zisikue kuzidi urefu wa sentimita mbili.
Zaidi ya hilo angalizo lilitolewa kwa wakorea Kaskazini kutoiga style ya nywele au unyoaji wa Kibepari.
Je utapenda nchi yako iweke sheria maalumu ya mitindo ya nywele kwa jinsia zote?
Makala hii imeandaliwa kwa Msaada wa vyanzo mbalimbali.



