
.
✍️ Yanga walianza game bila kuwa na idea yeyote ya ni nini wanatakiwa kukifanya , walikuwa na makosa mengi sana hasa wakiwa na mpira mguuni na hata bila mpira …. How ?
1: Wakati wanaanza Build Up wanalazimika kutumia long balls kusogea eneo la juu : Kwanini ? Kwasababu walishindwa kuivuka muundo mzuri wa Pamba kwenye kuzuia na 2-1 ( Washambuliaji wao wawili wanaweka presha kwa Job na Bakari then Najim anakuwa karibu na Conte dhumuni ni kuwanyima Yanga uhuru kwenye build up yao hasa kupita eneo la ndani .
2: Kama Yanga watafanikiwa kuivuka Build Up hiyo , wanakosa usahihi wa pasi zao kusogea eneo la juu ( wanapoteza sana mipira + muundo mzuri wa kuzuia kwa Pamba kwenye kiungo “Nashon na Mwashinga” na walifanikiwa kukabiliana vizuri na mashambulizi ya Yanga “BIG UP” .
3: Kuna nyakati unaona wachezaji wa Yanga hawakuwa na utayari kabisa kwenye kugombania mipira ya 50/50 ilikuwa tatizo , maamuzi yao ya mwisho hayakuwa sahihi , bila mpira hakuna pressing kuanzia eneo la mbele + Ufanisi mdogo mbele ya goli .
✍️ Nafikiri kocha wa Pamba Jiji “Fransis Baraza” alifanya homework yake vizuri sana dhidi ya Yanga ….. bila mpira wanakuwa na muundo wa 4-3-1-2 na walitoa wakati mgumu kwa Yanga + walikuwa wanafika kwenye maeneo kwa wakati sahihi …. Plan yao ya kushambulia ilikuwa kwenye Transition lakini walikuwa na idadi ndogo ya wachezaji eneo la juu .
✍️ Kipindi cha pili , Yanga walianza kufanya vitu vya kimsingi zaidi hasa wakiwa na mpira ( Hapo ndio wakaishinda game ) : usahihi wa pasi zao wakati wanashambulia, runner eneo la mbele , idadi nzuri ya wachezaji kwenye eneo la mbele na waliweka presha vizuri pale wasipokuwa na mpira .
NOTE :
1: Mohammed Doumbia alileta uhai kwenye kiungo ( Good Passer , Composure + mzuri kulinda mali )
2: Edmund John kacheza game bora sana Kasi , Skills na upambanaji : katoka na Assist kwenye mchezo wa leo .
3: Mohammed Hussein kacheza game nzuri sana + Assist …. Maxi Mpia ile Energy yake
4: Nashon na Mwashinga kwenye kiungo walicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza .
5: Bakari & Job ✅ ila yule Mwenda kaboresha sana game yake .



