
Klabu ya Simba imepata ushindi mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa dhidi ya Mashujaa kwenye dimba la Lake Tanganyika, iliwachukua Simba dakika 90+6 kuhakikisha wanaondoka na alama tatu.
Goli pekee la Simba limefungwa na Steven Mukwala aliyetokea benchi dakika ya 90+6 na kuwapa ushindi Wanalunyasi,
Simba wanasogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na alama 22 sawa na Singida BS ila wakiwazidi idadi ya magoli.
Mnyama Simba aendeleza Ufalme wake Mwituni.



